Jumatano, 25 Februari 2015

HALMASHAURI YA MASASI YAPUNGUZA KIASI CHA FEDHA KUTOKA MIRADI MINGINE ILI KUKARABATI BWAWA LA NANJOTA.

Halmashauri ya Masasi yapunguza kiasi cha fedha kutoka miradi mingine ili kukarabati bwawa la nanjota Halmashauri ya wilaya ya masasi mkoani mtwara imelazimika kupunguza fedha toka miradi mingine ya maendeleo ili kukarabati bwawa la nanjota ambalo limejengwa chini ya kiwango kupitia mradi wa tasafu awamu ya tatu kwa thamani ya shilingi milioni 75. Akizungumzia hatua hiyo katika kikao cha madiwani kilichokuwa kinajadili makisio ya bajeti kwa mwaka 2015-2016 mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Satmah amesema kikao hicho kimelazimika kupunguza fedha toka miradi mingine ya maendeleo shilingi milioni 30 katika bajeti ya mwaka 2014-2015 inayo ishia june mwaka huu,  ili kunusuru bwawa hilo lisiharibike ambalo linategemewa na vijiji zaidi ya vinne.    Miradi ambayo fedha zake zimepunguzwa ni pamoja na ujezi wa hospitali na ujenzi wa madarasa.   Akizungumzia ujenzi wa bwawa hilo diwani wa kata ya nanjota sehemu ambayo bwawa hilo limejengwa anasema wapo baadhi ya watendaji ndani ya halmashauri wamechangia bwawa hilo kujengwa chini ya kiwango, huku wananchi wa kata hiyo wakielezea kutoridhishwa na ujenzi huo.  ITV.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni