Ijumaa, 13 Februari 2015
NGUZO HII YA UMEME SI RAFIKI NA MVUA ZA DAR-ES-SALAAM.
Ni hatari ijayo lakini bado salama kwa sasa.Nguzo hii inawatia hofu wakazi wa eneo husika ambao macho na masikio yapo juu ya hatari hii ya nguzo japokuwa taarifa imekwishapelekwa mahali husika kwa muda mrefu tu lakini hamna utekelezaji wa hili.
Hofu iko pale mvua zitakapoingia kazini,je kuna dalili ya usalama au tunasubiri matukio ya kubeba walionusurika na waliopoteza maisha?
Hii ni Mbagala kizinga pembeni kidogo mwa kiwanda cha KTM.Wahusika!tuzibe ufa tusije jenga ukuta.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni