Jumatano, 11 Februari 2015
MNARA MREFU ZAIDI KATIKA MSITU WA AMAZON.
Nchi ya Brazil imeanza rasmi ujenzi wa mnara
mrefu zaidi duniani huko Manaus mjini Amazon.
Mnara huo kwa jina Amazon observation Tower,
unatazamiwa kutumika katika utafiti wa mapana wa
hali ya anga.
Utakuwa na vifaa maalum venye uwezo mkubwa
wa kukusanya data kuhusu gesi chafu iliyo hewani,
chembe chembe za erosoli na hali ya anga ya kila
uchao katika msitu wa Amazon.
Eneo hilo la Amazon ndilo linalinaloshuhudia mvua
kubwa zaidi kila msimu.
Wanasayansi wa Brazil na Ujerumani wanatumai
kuutumia mnara huu katika uchunguzi wao wa
vyanzo vya gesi chafu na mabadiliko ya hali ya
anga.
Kutokana urefu wake, mnara huu utawezesha
wanasayansi kuelewa mabadiliko ya mwelekeo wa
upepo kwa kitalifa cha zaidi ya kilomita mia moja
katika msitu wa Amazon.
Msitu wa Amazon umekuwa ukikatwa kwa muda
Msitu wa Amazon ni kati ya misitu mikubwa zaidi
duniani inayoathiri mazingira kwani inahusika
pakubwa katika kuongeza na kupunguza kiwango
cha hewa aina ya (carbon) angani.
Kulingana na bw. Paulo Artaxo, mwelekezi wa mradi
huo kutoka chuo kikuu cha Sao Paulo, amesema
mnara huo utasaidia pakubwa katika juhudi za
kutafuta majibu ya maswali mengi kuhusu
mabadiliko ya hali ya anga duniani.
Aidha, mnara huu unatarajiwa kutumiwa pamoja na
minara mingine midogo ambayo tayari imejengwa
nchini humo.
Kulingana na wajenzi, mnara huu utafanana na ule
uliojengwa Siberiaya katika mwaka wa 2006.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni