Jumatano, 18 Februari 2015

POLISI WANNE WAUAWA TUNISIA.

Tunisia imesema kuwa polisi wanne wameuawa kwenye shambulizi lilitokea katika mkoa wa Kasserine uliopo karibu na mpaka na Algeria. Wizara ya ndani ilisema kuwa tukio hilo lilifanyika eneo la Boulaaba. Shambulizi hilo lilifanyika eneo ambapo kundi lililo na uhusiano na mtandao wa Al Qaeda la (Okba Ibn Nafe'a) linaendesha harakati zake. Tunisia imeongeza ulinzi kwenye mpaka wake na Libya kufuatia kuzorota kwa usalama eneo hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni