Bunge la Ujerumani limeunga mkono kuongezwa kwa muda wa miezi minne zaidi kuisaidia Ugiriki kifedha.
Muda
uliridhiwa kuongezwa na wakopeshaji wa kimataifa juma lililopita baada
ya Ugiriki kuwasilisha mipango ya kufanya mabadiliko ya kiuchumi ambayo
yalitakiwa kuidhinishwa na Nchi wanachama wa Euro.baadhi ya Wabunge wa Ujerumani wameshuku kuhusu mpango huo ambao unaelezwa kuwa utaweza kupita kirahisi.
Hatua hii inakuja baada ya Polisi na Waandamanaji kupambana wakati wa Maandamano mjini Athens siku ya Alhamisi.
Hizi ni vurumai za kwanza tangu Chama cha Mrengo wa kushoto cha Ugiriki Syriza kuongoza Serikali kuu ya Ugiriki.
Wanaharakati waliwarushia mabomu ya Petroli na mawe Polisi na kuchoma moto magari baada ya Matembezi yaliyohusisha mamia ya Waandamanaji.
Mpango wa kupata mkopo pia umetikisa Chama cha Syriza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni