Jumatatu, 30 Machi 2015

MATOKEO YA UCHAGUZI NIGERIA LEO JIONI.

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni. Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi." Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega. Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo. Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.

BBC.

MATOKEO YA UCHAGUZI NIGERIA LEO JIONI.

Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni. Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura. Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega. "Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011. Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana. Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi." Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi."Tunaamini tumefanya vizuri kabisa. Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo. Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha. Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi, ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega. Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani. Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo. Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais, Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.

BBC.

FACEBOOK KUFUNGUA HUDUMA MPYA.

Mtandao wa facebook umethibitisha kwamba unafungua huduma yake ya messenger kwa wajenzi .Habari hizo zilitangazwa na Mark Zuckerberg katika kongamano la nane la wajenzi lililofanyika mjini San Fransisco.Zaidi ya programmu 40 mpya zikiwemo habari za hali ya anga tayari zimeandaliwa kwa huduma hiyo.Mtandao huo wa kijamii pia ulionyesha programu yake ya video inayomruhusu mtumiaji kusukuma kamera huku kanda hiyo ikicheza.

BBC.

ARSENAL KUMNUNUA WANYAMA NA MITROVIC.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga kumnunua kiungo wa kati wa Southampton Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa Anderlecht Aleksandr Mitrovic kulingana na gazeti la the Sun nchini Uingereza. Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20 naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic akigharimu pauni millioni 10. Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na kilabu kikubwa huku naye Mitrovic akiwa amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal katika kipindi cha wiki chache zilizopotea. Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier Drogba kutokana na mchezo wake.

Jumapili, 29 Machi 2015

RAIA WAANDAMANA KUPINGA UGAIDI TUNISIA.

Raia wa Tunisia wameandamana kupinga ugaidi nchini humo Serikali ya Tunisia inasema kuwa askari wa usalama wamemuuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji, lilohusika na shambulio la karibuni dhidi ya makavazi katika mji mkuu, Tunis, ambapo watu zaidi ya 20 waliuwawa. Waziri mkuu Habib Essid alisema, raia wa Algeria, kwa jina Lokman Abu Sakhra ambaye ameelezewa kuwa gaidi hatari kabisa nchini humo aliuwawa, pamoja na wapiganaji wengine wanane, kwenye shambulio lilofanywa katika jimbo la Gafsa, magharibi kwa nchi. Wapiganaji hao ni wa kundi liitwalo Ibn Nafaa Brigade. Maelfu ya watu wameshiriki kwenye mha-dhara wa mshikamano, kupinga ugaidi. Watu maarufu walishiriki kwenye mhadhara huo, pamoja na wageni mashuhuri, akiwemo Rais François Hollande wa Ufaransa, Waziri mkuu wa Itali, Matteo Renzi, na kiongozi wa Wa Palestina, Mahmoud Abbas.

BBC.

UPIGAJI KURA WAENDELEA NIGERIA.

Shughuli ya kupiga kura yaendelea katika maeneo kadhaa nchini Nigeria Katika uchaguzi mkuu wa Nigeria, watu wanaendelea kupiga kura kwa siku ya pili katika baadhi ya vituo, kwa sababu ya matatizo ya kiufundi yaliyotokea jana. Vifaa vya kusoma vitambulisho, vilivyokusudiwa kuzuia udanga-nyifu, viliharibika, na kuchelewesha upigaji kura. Lakini katika maeneo mengine, mamilioni ya wa Nigeria walipiga kura bila ya tatizo. Mashindano ni makali baina ya wagombea wawili wakuu wa urais, Goodluck Jonathan na kiongozi wa zamani wa kijeshi, Muhammadu Buhari. Wanajeshi wa Nigeria hivi sasa wanapambana na wapiganaji kadha wa Boko Haram, nje ya mji wa Bauchi, kaskazini-mashariki mwa nchi.

BBC.

Jumamosi, 28 Machi 2015

SIMBA YAGUNDUA UCHAWI WA MSUVA.

WAKATI Simba wakiweweseka na kasi ya mabao aliyonayo Simon Msuva wa Yanga, kinara huyo wa mabao wa Ligi Kuu ni kama amewafichulia siri yake. Msuva mwenye mabao 11, matano kati ya hayo akiyafunga kwa kichwa, mawili kwa penalti na manne kwa mguu alifichua kuwa wala si uchawi kama watu wanavyofikiria bali ni ujanja wake wa kuiba muda wa kocha wake, Mholanzi Hans Pluijm wanapokuwa mazoezi ili kujifunza kufunga ndiyo sababu ya kumfunika Didier Kavumbagu mwenye mabao 10. Aliweka wazi kuwa, amekuwa akiwasumbua, Juma Abdul na Mnyarwanda Mbuyu Twite mara kwa mara wampigie mipira ya krosi na yeye amalizie kufunga kwa kichwa au mguu huku makipa, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’ akiwaomba wakae golini. Alisema, amekuwa akifanya hivyo karibu kila kipindi cha mazoezi na kila mmoja amekuwa anamwomba ampigie mipira mitano au sita na  kwa upande wa makipa mbali na kuokoa mipira hiyo ya krosi, huwa anawapigia mipira mingine mitano ya penalti kila mmoja. Akizungumza na Mwanaspoti, Msuva alisema: “Ninatamani kufunga, napenda nifunge na hamu yangu ni kufunga lakini pale ninapoweza faida ya klabu na mimi mwenyewe, nikawa nafanya sana mazoezi ili nifanikiwe.” “Nimekuwa nikiwasumbua sana baadhi ya wachezaji mazoezini, huwa naibia mwalimu anapokuwa amesimamisha programu yake kwa muda mfupi, huwa nawaomba wanipigie krosi na mimi nijaribu kufunga kwa kichwa na miguu makipa wakiwa golini. Wakati mwingine nawaomba pia wachezaji wa katikati wanichezeshee mipira nayo nafunga ni hivyo tu,” alisema Msuva ambaye amefunga mabao ya kichwa katika mechi waliyocheza na Prisons mzunguko wa kwanza bao moja, raundi ya pili mawili dhidi ya Prisons, moja na Mbeya City na moja dhidi ya Azam. “Lakini pamoja na hamu yangu hiyo, huwa silazimishi kufanya hivyo, ninapokuwa sina uwezo, pia namwomba Mungu anilinde na majeraha ili nitimize malengo yangu ya kufunga kadri niwezavyo ili niwe mfungaji bora na timu yangu ichukue ubingwa.” Msuva ambaye kuna habari kwamba Simba inamuwania pia aling’ara kwa mabao kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi ambalo hata hivyo ni mahasimu wao Simba ndio waliobeba taji la michuano hiyo.

REKODI

Awali Msuva alikuwa anacheza straika wa kati katika klabu mbalimbali alizopitia kama, Azam FC, Moro United na timu za Taifa za vijana chini ya miaka 17 na 20. Baada ya kutua Yanga, alihamishiwa pembeni nafasi ya winga na yeye anasema: “Sina tatizo kucheza nafasi hiyo, kama una uwezo wa kufunga mabao, kokote utafunga iwe straika wa kati au winga pembeni.” Kocha wake mkuu, Mholanzi Hans Pluijm amesifu kiwango cha Msuva kuwa ni mchezaji anayefuata maelekezo na kukubalia mabadiliko. Umahiri wa Msuva unakaribiana na ule waliokuwa nao wachezaji Mrisho Ngassa na Mussa Hassan Mgosi ambao ni mawinga, lakini walioweza kunyakua tuzo ya Ufungaji Bora katika Ligi ya misimu ya nyuma kwa kufunga mabao 16 kila mmoja katika msimu wake. Kasi hiyo ya Msuva kwa mechi saba zilizosalia kwa timu yake kabla ya kufunga msimu inaweza kumfanya amfikie aliyekuwa Mfungaji Bora msimu uliopita Amissi Tambwe aliyefunga mabao 19. Hata hivyo, uwiano wake wa mabao unampa wakati mgumu kufikia rekodi hiyo ya Tambwe aliyemzidi mabao mawili Kipre Tchetche aliyekuwa kinara wa mabao msimu wa 2012-2013.

GUMZO MWANZA

Wakati nyota wa Yanga wakitua jijini hapa kwa ajili kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kucheza na Malawi kesho Jumapili, Msuva amekuwa gumzo midomoni mwa mashabiki wa soka wa Mwanza baada ya kutoonekana kwenye mazoezi na wenzake. Mashabiki wameingiwa na mchecheto na kuhoji alipo Msuva na kudai kama hatakuwemo ni wazi Malawi itakuwa na kazi rahisi kushinda. Wachezaji wa Yanga walionekana kambi ya Stars ni Oscar Joshua, Nadir HaroubCannavarona Mrisho Ngassa waliotua juzi Alhamisi, walipasha kidogo uwanjani kabla ya kuondoka na gari la Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba na Kocha wa Toto Africans, John Tegete. “Tumefurahi kuwaona nyota wa Yanga wakijumuika na Stars, lakini hatujaridhika na tuna mashaka makubwa kwani hatujamuona Msuva na muda wa mazoezi ni mdogo sijui kama wataweza kuwahimili wa Malawi,” alisema Selemani Mashimba. Hakuna kiongozi wala kocha aliyekuwa tayari kuzungumza jambo lolote la timu hiyo kwa madai watazungumza siku moja kabla ya mchezo. Katika mazoezi ya juzi ya mashabiki iliongezeka na kama Chama cha Soka Mwanza (MZFA) wangeamua kuwatoza kiingilio cha Sh1000 basi wangepata pesa za maana. Mashabiki wengi walikuja ili kuwaona nyota hao wa Yanga tofauti na hali ilivyokuwa katika mazoezi yaliyopita. Hata hivyo, wakati mashabiki wakiwa na hamu na Msuva, strika Mbwana Samatta aligeuka kivutio kikubwa kwenye upigaji wa penalti  katika mazoezi hayo ya juzi baada ya kumtungua Mwadini Ally kwa mikwaju saba jambo lililomfanya kipa huyo abaki akicheka tu.

GAZETI MWANASPOTI.

Ijumaa, 27 Machi 2015

YANGA YAMJAZA UPEPO STRAIKA WA SIMBA.

VIONGOZI wa Simba, wamegundua kwamba walibugi kumpiga chini straika wao namba moja wa msimu uliopita, Amissi Tambwe ambaye sasa anatamba na kuwapa kiburi Yanga kutokana na uwezo wake wa kutupia kwenye nyavu. Vigogo hao wameingia msituni kumsaka mchezaji huyo kwa udi na uvumba ili arudi Msimbazi haswa baada ya Kocha Mserbia, Goran Kopunovic kuwaambia mabosi wake kwamba mchezaji huyo bado ni kifaa na anamhitaji. Lakini Yanga wamemuweka chini Tambwe na kumwambia atulie watampa maisha bora na kitendo cha timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa ndicho kimempagawisha zaidi aendelee kubaki Jangwani ambapo amemhakikishia Kocha Hans Pluijm kwamba harudi Simba hata kwa dawa. Akizungumza na Mwanaspoti, Pluijm ambaye ni Mholanzi, amesema amezungumza na Tambwe juu ya maisha yake ya baadaye ambapo raia huyo wa Burundi amemhakikishia kwamba hawezi kurudi Simba msimu ujao. Pluijm alisema Tambwe ambaye mpaka sasa ameshaifungia Yanga mabao saba katika mashindano ya aina mbili bado ni mchezaji muhimu katika kikosi chake baada ya kukubalika katika mfumo wa timu hiyo. “Nimesikia hizo taarifa kwamba kuna watu wanataka kumrudisha Simba, nikazungumza na Tambwe na amenihakikishia kwamba hawezi kukubali kurudi huko tena kwani anafuraha akiwa hapa na timu yetu, jambo zuri ni kwamba Tambwe ni mchezaji wetu anayefanya vizuri nafurahia anavyojituma katika timu ameweza kufanya kile ambacho makocha tunamtaka afanye uwanjani, katika hilo unawezaje kumruhusu mtu kama huyo aondoke katika timu yako?” alisisitiza Pluijm. Hata ushiriki wa Yanga kwenye michuano ya kimataifa umemfanya mchezaji huyo kutuliza akili Yanga kwa madai kwamba mbali na kushiriki msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho hata mwakani kuna uwezekano mkubwa wa kushiriki tena huku nafasi ya Simba ikiwa finyu kutokana na kuchechemea kwenye ligi ya ndani. “Sijajua kwa nini Tambwe aliachwa, anafanya vizuri tunahitaji mtu kama huyo katika timu yetu, ukiangalia kwa sasa tuna mtu mmoja tunayemtegemea katika ufungaji Okwi, anakosa msaidizi, namjua vyema Danny (Sserunkuma ) lakini ameshindwa kufanya vizuri,”alisema Kopunovic. “Nilikuwa mshambuliaji, namjua mshambuliaji mzuri, angalia Chelsea walikuwa na shida ya ufungaji wakamsajili Diego Costa sasa anafunga, siku zote mchezaji mzuri ni yule anayefanya vizuri katika wakati husika,”alisisitiza kocha huyo ambaye kuna uwezekano mkubwa akamtema Sserunkuma ambaye tayari ameshaomba kupunguza urefu wa mkataba wake aondoke Simba baada ya mambo kutomwendea vizuri.

GAZETI MWANASPOTI.

Alhamisi, 26 Machi 2015

A GIRL WITH POSITIVE IDEA.

My boyfriend and I both have a lot on our plates. He with his work, which is crazy intense, and me with my work and studying for licensure. Despite all this pressure and chaos, we still make time for each other on the weekends and a few hours throughout the week. We both commented on that fact tonight how despite everything we are still going strong. I guess we're important to one another and both willing to find a way rather than finding an excuse to run away.

NINI KILIIKUMBA NDEGE YA UJERUMANI?

Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps. Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo . Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika. David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege ,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini kilichotokea . pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu,na hatua walizochukua kunusuru janga hilo. Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea kurusha ndege? Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na nini walichokiacha na mambo kama hayo. nini kilitokea? swali halina jibu,kisanduku cheusi kimeharibika Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa taarifa ili tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea. Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Carsten Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Germanwings shirika dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea ajali hiyo kuwa isiyoeleweka. niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika tasnia hii nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa,bado hainiingii akilini juu ya kile kilichotokea jana. Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi kupoteza ndege yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama hayo ,bado hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali nzuri kiufundi na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia mafunzo ya hali ya juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa,kuhusika katika ajali mbaya kiasi kile .

BBC.

MAREKANI:Uganda hatarini kushambuliwa.

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo. Aidha Marekani pia imetoa tahadhari kwa raia wake. Taarifa ya ubalozi huo umebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana. Katika kipindi kilichopita, kundi la Al-Shaabab lenye makao yake Nchini Somalia, limetekeleza mashambulio Nchini Uganda.

BBC.

Jumatano, 25 Machi 2015

NIGERIA YAKIRI KUTEKWA NYARA RAIA.

Serikali ya Nigeria imekiri kwamba raia,wakiwemo watoto wametekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram katika majuma ya hivi karibuni. Msemaji Mike Omeri amesema kuwa ni vigumu kukisia idadi ya watu ambao wametekwa wakati wapiganaji wa Boko Haram wakitoroka wakati wa mashambulizi dhidi yao yanayotekelezwa na vikosi vya kijeshi kutoka Nigeria,Chad na Niger. Lakini msemaji wa Nigeria alipinga madai kwamba zaidi ya watoto 500 walikuwa hawajulikani waliko kutoka mji uliochukuliwa na jeshi Damasuk karibu na mpaka wa Niger. Nigeria imetangaza kwamba inafunga mpaka wake kuanzia siku ya jumatano usiku hadi jumapili huku uchaguzi wa urais ukifanywa.

BBC.

MABIBI HARUSI WA ZAMANI ZIMBABWE WAONGEA.

Mabibi harusi wa zamani wawili wameamua kuipeleka serikali ya Zimbabwe mahakamani katika harakati za kuvunja sheria kandamizi nchini humo na kutaka sheria inayoruhusu mabinti kuolewa wakingali wadogo iwe ni kinyume na katiba na si halali kwa kifupi iharamishwe. Mabibi harusi hao Loveness Mudzuru na Ruvimbo Tsopodzi wamesema ndoa za utotoni ,ambazo ni ruksa nchini Zimbabwe,wansema ni sawa na ukatili wa kijinsia kwa watoto ambao huwanasa mabinti na kuishia katika janga la umasikini na madhila yasiyosemeka. Nimekabiliana na changamoto zisizosemeka ,mume wangu alikuwa akinipiga sana.nilikuwa natamani kuendelea na masomo lakini yeye alikataa.nilikuwa na hali mbaya sana huu ni ushuhuda wa Tsopodzi, mama wa mtoto mmoja,mama huyu aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitano tu . Na anaendelea kusema kwamba anataka kuchukua hatua hiyo ili kuleta tofauti,ameeleza hayo akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare mapema wiki hii.Na hii yote ni katika harakati za kuzuia mabinti wadogo wanaoolewa katika umri mdogo. Takwimu zilizochapishwa mwaka wa jana zinaonesha kwamba moja ya tatu ya wasicha walio na umri wa chini ya miaka kumi na nane huolewa , wakati wengine wapatao asilimia tano huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka kumi na mitano. Katika tamko lao kwa mahakama ya katiba, Tsopodzi na Mudzuru, ambao kwa sasa wana miaka 19 na mwingine ana miaka 20, wanasema kwamba sheria ya ndoa nchini Zimbabwe ni ya kibaguzi kwani inamtaka mtoto wa kike aolewe akiwa na umri wa miaka kumi na sita wakati mtoto wa kiume anatakiwa kuoa akishatimiza umri wa miaka kumi na nane, na ndoa za kimila hazijaainisha umri halisi wa kijana ama binti kuoa ama kuolewa. Sheria ya ndoa ya mwaka 2013 inasema kwamba kila mtoto mwenye umri wa miaka kumi na mitatu,anayo haki ya kupata malezi ya wazazi,elimu na ulinzi kutoka kwao katika masula ya unyonyaji kingono na kiuchumi. Sheria hii pia haijaweka wazi umri wa kuoa ama kuolewa lakini inasisitiza kwamba hakuna mtu yeyote atakayelazimishwa kuoa ama kuolewa kinyume na matakwa yao na kuonesha wazi kuwa raia wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka kumi na nane anaweza kuwa na familia yake. Umasikini ndio chanzo cha ndoa za utotoni nchini Zimbabwe na kuwasababisha kuolewa kabla ya umri wao wasichana walio wengi ,na hivyo kuwasababisha wazazi kupunguza mzigo wa familia katika masuala ya matunzo na kubakisha mama tu na baba.ulipwaji mahari nayo ni motisha inayowafanya wazazi kutowatendea haki watoto wao. Baadhi ya familia nchini Zimbabwe zinatukuza ndoa za utotoni kwa mtazamo wa kuwalinda watoto wao wa kike na ngono kabla ya ndoa. Mudzuru anatoa ushuhuda wake kwamba ndoa za utotoni ni chagamoto kubwa ,kwani mabinti hao walio katika umri mdogo watazaa watoto wakiwa katika familia masikini na hapo ndipo mzunguuko wa ndoa za utotoni unapoanza upya. Mudzuru, aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na sita kwa sasa ana watoto wawili tena akiwa hajatimiza miaka kumi na nane ,anasema maisha yake yalikuwa sawa na jehanamu ya moto na aliishi maisha yake katika dhiki isiyosemeka. Nasema maisha yake yalikuwa magumu sana, kulea watoto ilhali wewe mwenyewe ukiwa ni mtoto ni vigumu,na asema katika umri wake alipaswa kuwa anahudhuria masomo shuleni. Naye mwanasheria wa mabinti hao ambao ni akina mama sasa hivi,alikuwa ni waziri wa zamani wa fedha nchini humo Tendai Biti, aliwasilisha changamoto hizo za kisheria mwezi January mwaka huu. Beatrice Savadye,yeye ni mwanaharakati wa kupinga ndoa za utotoni nchini humo anayeongoza asasi isiyokuwa ya kiserikali,ijulikanayo kaka ROOTS ,asasi ambayo inawaunga mkono akina mama hao wawili anasema kesi hiyo imekuwa na mvuto wa kipekee nchini humo nan je ya nchi hiyo kwa ujumla wake. Na anamashaka kama mahakama itatoa maamuzi yake lini ,lakini inalazimika kutoa maamuzi yake ndani ya miezi sita. Ulimwenguni kwa ujumla wake wasichana milioni kumi na tano wanaolewa kila mwaka.katika jangwa la sahara peke yake asilimia arobaini ya wanawake huolewa wakiwa katika umri mdogo.

BBC.

ROBO YA WASUDAN KUSINI WAMEATHIRIKA NA NJAA.

Robo ya wasudan Kusini wameathirika na njaa Shirika la chakula ulimwenguni linasema njaa inaongezeka kwa kasi nchini Sudan Kusini baada ya miezi mingi ya mapigano. Zaidi ya watu milioni mbili unusu wanahitaji chakula cha msaada cha dharura, baada ya kufurushwa makwao kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na vikosi vya waasi. Mazungumzo ya kuleta amani yaliyokuwa yakiendelea katika taifa jirani la Ethiopia, yamesambaratika. Haya yanajiri siku moja tuu baada ya bunge kumuongeza rais Salva Kiir miaka mitatu zaidi afisini na kuhairisha uchaguzi uliotarajiwa mwaka huu. Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anaelezea zaidi. Hapa ni katika mji wa Ganyiel kwenye jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Unity, maelfu ya watu waliofurushwa makwao wamefika katika kituo cha Shirika la WFP ambapo wanapata mtama, mafuta na chumvi. Kwa wengi hapa msaada huo ndio chakula cha pekee wakatachopata. Shirika la WFP linasema mtu mmoja kati ya wane nchini humo, hawajui watapata wapi chakula Nchi hii iliepuka kiangazi mwaka uliopita, lakini bado hakuna chakula cha kutosha. Asilimia kubwa ya raia wa Sudan Kusini wanahitaji chakula cha dharura WFP inasema watu milioni mbili unusu wanahitaji msaada wa dharura na idadi hiyo huenda ikaongezeka mara mbili kufikia katikati ya mwaka huu, iwapo mapigano yataendelea. Miongoni mwa wanaopanga foleni hapa kutafuta chakula ni Elizaberth Nyalat aliyetoroka mapigano katika mji wa Nyalat, Kusini Magharibi mwa Nchi hiyo. "nilikuwa nasomea mjini Yei, wakati vita vilipoanza. Nilitoroka Yei hadi hapa. Lakini sio kwa gari wala boti, nilikimbia kwa miguu. Ilikuwa ngumu sana kwangu kufik amahali hapa." Lakini amani hiyo imekuwa ngumu kupatikana. Baada ya miezi kumi na mitano ya mapigano yaliyofanya maeneo mengi kaskazini mwa nchi hiyo kuwa numu kuyafikia. Na sasa mashirika ya kutoa misaada yako mbioni kutoa usaidizi kabla ya msimu wa mvua kuanza. Ertharin Cousin ni mkurugenzi Mkuu wa WFP "watu milioni tatu tunaojaribu kuwafikia,sio tu takwimu ni watu wa kweli. Tatizo ni kuwa , vita hivi vinavyoendelea kwa muda mrefu, ndivyo watu hawa wanasahaulika na kutazamiwa tu kama gharama au takwimu tu. Lakini haya ni maisha ya watu. Ni binadamu." Awamu mpya ya mazungumzo ya amani yanatarajiwa kuanza tena mwezi ujao...lakini huenda ikaathirika na hatua ya bunge hapo jana kumuongezea Rais Kiir miaka mitatu zaidi mamlakani. Uchaguzi wa mwezi Juni pia umeahirishwa. Upinzani hata hivyo unasema hatua hiyo ya Kiir ni sawa na kukwamilia mamlaka. Na huenda ikavuruga juhudi nzima ya kuleta amani nchini humo. Hali hii ya swintofahamu huenda sasa ikamaanisha kuwa kambi za wakimbizi wa ndani kwa ndani zitasalia kuwa makao kwa raia wengi wa Sudan Kusini kwa kuda mrefu zaidi.

GAZETI MWANASPOTI.

KOCHA KOPUNOVIC ASIMULIA MAAJABU YA OKWI SIMBA.

KOCHA wa Simba Goran Kopunovic ametamka kwamba kikosi chake kimejaliwa wachezaji wengi wenye KOCHA wa Simba Goran Kopunovic ametamka kwamba kikosi chake kimejaliwa wachezaji wengi wenye vipaji, lakini ndani yake kuna mchezaji mmoja tu mwenye maajabu akimtaja ni Emmanuel Okwi. Kopunovic raia wa Serbia alisema Okwi amekuwa na maajabu ya hali ya juu katika kikosi hicho hasa katika ushindi wa mechi tatu zilizopita ambazo zimethibitisha ubora wake ndani ya timu hiyo. Alisema mabao hayo mawili aliyoyafunga yanatokana na akili iliyotulia aliyonayo mshambuliaji huyo akiwataka wachezaji wengine kuiga. “Anajua nini afanye uwanjani hasa kunapokuwa na mazingira magumu, huo ndiyo ubora wa Okwi ni mchezaji wa kipekee ingawa kuna wengine bora pia,”alisema Kopunovic. “Angalia haya mabao aliyoyafunga katika mechi hizi (dhidi ya Yanga na Mtibwa), kazi kama hii hufanywa na wachezaji majasiri.” Naye mtoto wa Kopunovic aitwaye Denis aliyezaliwa miaka 12 iliyopita aliungana na baba yake kumwagia sifa Okwi. Denis anayeichezea timu moja ya vijana huko Hungary alisema: “Yule mwenye jezi namba 25 ni hatari sana anajua kuwapunguza mabeki angalia anavyobaki na beki mmoja anavyomfanya, anaweza kucheza Ulaya yule.

GAZETI MWANASPOTI.

Jumatatu, 23 Machi 2015

ULIMWENGU WAOMBOLEZA KIFO CHA LEE YEW.

Yew aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 91 Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia. Lee amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa mapafu. Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha kimataifa. David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini humo, ametuma salamu zake za rambi rambi. Kifo cha Lee ni mwisho wa enzi zake. mwisho wa mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani katikati ya miaka ya sitini . Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata leo na unaweza kuvuka mipaka sio kwa singapore tu bali hata kwa watu wa Asia ya kusini Mashariki. Viongozi mbalimbali duniani wanaendelea kutuma risala za rambirambi kwa Singapore, baada ya kifo cha Lee Kuan Yew hospitalini. Yew aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua homa ya mapafu. Nchini Uchina, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imemsifia na kumtaja Lee Kuan Yew, kama kiongozi wa kipekee wa bara Asia. Marehemu Lee ambaye aliiletea mabadiliko makubwa taifa la Singapore na kuwa na mojawepo ya bandari maarufu zaidi Duniani huku uchumi wa nchi hiyo ukiimarika maradufu, atasalia katika kumbukumbu la taifa hilo. Mwanawe ambaye ni waziri mkuu wa sasa nchini humo, Lee Hsien Loong, anasema kuwa Singapore haitawahi kuwa na mtu kama huyo tena. Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani Katika risala zake za rambirambi, Rais Barrack Obama wa Marekani amemtaja kama gwiji wa historia. Nchini Uchina, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imemsifia na kumtaja Lee Kuan Yew, kama kiongozi wa kipekee wa bara Asia. Naye waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, anasema kuwa Bwana Lee alikuwa mmojawepo wa viongozi wakuu duniani. Serikali ya Singapore imetangaza siku sita ya maombolezo, hadi atakapozikwa siku ya Jumapili.

BBC.

MTO NILE;MISRI ETHIOPIA NA SUDAN ZAPATANA.

Misri, Ethiopia na Sudan zimetia saini mkataba wa kwanza kuhusu ugavi wa maji katika ya Nile unaopitia mataifa hayo yote matatu. Mkataba huo unafuatia ujenzi unaoendelea wa bwawa kubwa la ''the Grand Rennissance'' linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile. Ujenzi huo umezua mzozo mkali wa kidiplomasia kati ya Misri na Ethiopia. Mwandishi wa BBC nchini Ethiopia Emmanuel Igunza na maelezo zaidi. Viongozi wa mataifa hayo matatu,walikutana jijini Khartoum Sudan kwa sherehe ya kutia saini mkataba huo ambao umetajwa kama hatua ya kwanza katika kutatua mzozo huo. Bwawa hilo linalotarajiwa kugharimu takriban dola bilioni nne, litakamilishwa mwaka wa 2017 na kuwa moja ya mabwawa kubwa zaidi barani Afrika. Ethiopia inasema itaisaidia katika kuzalisha nguvu za umeme kwa ajili ya viwanda vyake na pia inatarajia kuuza kawi kwa mataifa jirani. Lakini akizungumza hii leo, Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi amesema mkataba huo unashiria nia ya mataifa yote kuleta maelewano kuhusu utumizi wa maji ya mto Nile. Abdel Fattah Al Sisi alisemaMradi huu wa bwawa la renaissance linashiria chanzo cha maendeleo kwa mamilioni ya raia wa Ethiopia kwa kuzalisha kawi safi, lakini kwa ndugu zao wanaoishi katika kingo za mto huohuo wa Nile nchini Misri, na mabo idadi yao ni sawa, inashiria chanzo cha wasiwasi. Hii ni kwa sababu Nile ndio chanzo chao ha peke cha maji, na hasaa chanzo cha maisha.” Ethiopia inasema itaisaidia katika kuzalisha nguvu za umeme kwa ajili ya viwanda vyake Mara kwa mara Misri imepinga mradi huo ikisema huenda bwawa la Rennaissance likapunguza viwango vya maji kwa raia wake. Hata hivyo Rais wa Sudan Omar al Bashir ametaka mataifa yote matatu kuhakikiha yanazingatia maendeleo lakini pia kutilia maanani maslahi ya nchi zote. “Tunamini kuwa ushirikiano ndio njia ya pekee ya kuafikia maelewano na utangamano kati ya watu wetu, na kwamba bila ushirikiano, tutapoteza nafasi ya kuwa na masiha bora. Kwa hivyo tunahitaji kufanya kazi pamoja kujenga mazingira ya ushirikiano na kukariri kwa maslahi ya kitaifa hayageuki na kuwa vikwazo kwa maslahi za kikanda na ujirani mwema.” Alisema rais Bashir Ethiopia ilianza kubadilisha mkondo wa mto Nile mwezi Mei mwaka wa 2013, ili kujenga bwawa hilo linalotarajiwa kuzalisha megawati 6,000 za umeme litakapokamilika. Misri kwa upande wake inaamini kuwa ina haki za kihistoria za mto huo kufuatia mikataba ya mwaka 1929 na 1959, inayoipa asilimia 87 ya maji ya mto huo, na pia uwezo wa kupinga miradi yoyote inayojengwa katika mto Nile.

BBC.

SIMBA KUTEMA MIZIGO.

KLABU ya Simba ipo mbioni kuwatema wachezaji ambao wameonekana mzigo ndani ya klabu hiyo katika msimu huu. Habari za ndani zimewataja wachezaji hao ni pamoja na Simon Sserunkuma aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili wa klabu hiyo mwishoni mwa mwaka jana. Wengine ni walioshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza karibu msimu mzima na kuoneakana wana kula mshahara na posho bure. “Kamati ya Usajili ilikutana mwishoni mwa wiki na kuwajadili wachezaji hao mizigo na wameamua mwishoni mwa msimu waachwe hasa wale waliomaliza mikataba yao na wenye mikataba mirefu watasitishwa,” kilisema chanzo chetu. Kiliongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha msimu ujao Simba inaunda kikosi imara kwa kusajili wachezaji watakaokuwa msaada kwa timu yao tofauti na sasa wakisuasua na kutokuwa na hakika ya kurejesha taji la Ligi Kuu linaloshikiliwa na Azam na linalowaniwa pia na watani za Yanga. Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspoppe, alikanusha kuwepo kwa mipango hiyo, licha ya kukiri kukutana kuwajadili wachezaji wao. “Hatukukutana ili kujadili wachezaji wa kuwaacha, tulikutana kuwajadili wachezaji waliomaliza mikataba yao kwa lengo la kuona tunafanya nini kwa ajili ya msimu ujao,” alisema Hanspope na kuongeza kwamba uamuzi uliofikiwa katika kikao hicho ni kuwaongezea mikataba mipya wachezaji hao ingawa Mwanaspoti linajua kwamba wengi watatemwa.

MIKATABA YA OWINO,NDEMLA YAFUTWA YANGA,MSUVA STOP.

KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm, ambaye ni miongoni mwa makocha wachache wenye misimamo kwenye Ligi Kuu Bara, ameapa kwamba ndani ya mkataba wake na Yanga, si Said Ndemla, Joseph Owino, Ivo Mapunda, Haroun Chanongo, Amri Kiemba wala Shabaan Kisiga hakuna atakayevaa jezi ya Yanga. Wachezaji hao sita wanamaliza mikataba yao na Simba msimu huu na mpaka sasa hawajaongezewa huku viongozi wa Mnyama wakihofia kwamba Yanga inaweza kuwatia kitanzi muda wowote mastaa wao wawili; Owino na Ndemla. Kocha huyo ambaye viongozi wa Yanga wametokea kumwamini sana amesisitiza kwamba pia hataruhusu kiungo mshambuliaji wao, Simon Msuva kusajiliwa na Wekundu wa Msimbazi. “Msuva namjua vyema kuliko mashabiki wanavyomjua najua umuhimu wake, lakini pia najua mapungufu yake ukiangalia yanazidi kupungua muda unavyozidi kwenda,ni mchezaji anayehitajika hapa Yanga ni vyema sasa mashabiki wakamuacha acheze aisaidie timu, nikiwa hapa Yanga siwezi kufanya kosa la kumuacha aondoke hasa kwenda Simbam,” alisema. “Nimepanga jambo moja nikiwa kocha wa Yanga, sitasajili mchezaji yeyote kutoka Simba hata awe na ubora kama Lionel Messi wa Barcelona, nimegundua jambo moja hata wakija hapa hawaaminiki na watu wa Yanga ni vyema tukasajili kutoka timu zingine lakini sitasajili kutoka Simba.” Kauli hiyo ya kocha huyo amezima ndoto za mastaa hao wa Simba kupewa mikataba na Yanga kwani hata uongozi wa juu umeonywa na wanachama kwamba wasisajili mtu yeyote kutoka Simba kwa vile hawana msaada na wanafanya Yanga inakuwa mteja kwa Simba kila wanavyokutana katika mechi zao. Wanachama matajiri wa Yanga wamekuwa na tabia ya kununua wachezaji mahiri wa Simba kila inapofika mwisho wa msimu ili kudhohofisha wapinzani wao, lakini hali hiyo huenda mwaka huu ikashindikana mpaka mkataba wa Pluijm utakapomalizika mwishoni mwa mwaka ujao na hata ukimalizika huenda akaongezwa kama ufanisi wake ukiimarika. Katika hatua nyingine, Yanga juzi Jumammosi walitumia Sh5 milioni ndani ya saa tatu kuwanunulia viatu maalumu wachezaji kwenye mechi dhidi ya Mgambo JKT iliyopigwa Tanga na Yanga kushinda mabao 2-0. Hiyo ilitokana na Uwanja wa Mkwakwani,Tanga kujaa matope kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku moja kabla ya mechi hiyo. Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano, Mhandisi Isaac Chanji, ambaye aliambatana na mjumbe wake katika kamati hiyo, Yusuphed Mhandeni na Katibu wa timu hiyo Dk. Jonas Tiboroha, mabosi hao walilazimika kutumia kiasi hicho kununua viatu hivyo maalumu ambavyo vilitumiwa na wachezaji kupata ushindi huo muhimu. “Kweli walinunuliwa viatu, isingekuwa rahisi kupambana na viatu vya kawaida katika uwanja kama ule, lakini sio wote waliovitumia kuna wengine walitumia vyao,” alisema Pluijm.

Jumamosi, 21 Machi 2015

JE ULIANDIKA LINI MWISHO BARUA YA MAHABA?

Idhaa ya utangazaji ya BBC leo imezindua mradi wa kimataifa unaohusisha wanafunzi katika utangazaji wa habari. Wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia wamepata fursa ya kuandaa ripoti kuhusu maswala mbalilmbali yanayowahusu. Kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi tunakuletea ripoti iliyoandaliwa na wanafunzi wa shule ya upili ya wavulana ya Starehe ambapo hawaruhusiwi kubeba simu za mkononi shuleni. Karibu katika shule ya Starehe boys centre mjini Nairobi. Shule yetu inajulikana kwa umahiri katika masomo hasa katika mitihani ya kitaifa. Ili kuimarisha umakinifu wetu masomoni, haturuhisiwi kubeba simu shuleni. Tuna vyumba vya computa vyenye internet lakini tunavitumia tu kwa masomo na utafiti peke yake. Haturuhusiwi kutumia computa kwa mawasiliano kupitia barua pepe au mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter. Lakini hilo halituzuii kuwasiliana na marafiki zetu hasa wasichana katika shule zingine. Matumizi ya simu yamepelekea watu wengi kusahau uandishi wa barua Inatubidi kutumia njia ya zamani,tunaandika barua,lakini sio barua za kawaida. Ni barua zilizoandikwa kwa umakinifu na kurembeshwa kwa kalamu zenye rangi aina mbalimbali na hua tunaziandika wakati wa mapumziko. Katika maktaba ya shule nakutana na baadhi ya marafiki zangu wakiandika barua baada ya masomo. ''Mara nyingi tunaandika barua hizi kwa marafiki zetu wasichana kwa hivyo tunaziandika kwa njia spesheli ili kupasha hisia zetu sawasawa'', anasema Charles huku akitabasamu. Baadhi ya wanafunzi wanaamini kuandika barua ni njia bora kwani inawapa fursa kutumia vipaji vya usanii.'' Napenda sana sanaa ya uchoraji na pia matumizi ya lugha hasa ya mapenzi '', anasema Moses huku akirembesha bahasha kwa kutumia kalamu zenye rangi tofauti. Kwa mpenzi wangu .... ''Namwandikia rafiki yangu wa karibu sana nilimuona mara ya mwisho wakati wa likizo na nahisi nimemkosa sana'', anaongeza. Baada ya kuandika barua hizo, tarishi anatumia pikipiki yake kuzisafirisha hadi katika shule ya wasichana ya Loreto Msongari, upande mwingine wa mji. Wasichana wanafurahia kuzipokea na baadhi yao wananieleza fikra zao kuhusu matumizi ya barua kama njia ya kuwasiliana. ''Nimependezwa sana na barua niliyopokea ,imerembeshwa kwa rangi aina mbalimbali'' anasema Stacy. '' Nafikiri ni bora kutumia barua kuwasiliana kwasababu njia zingine kama simu zinaweza kutufanya tusizingatie masomo'', anaongeza. Wasichana kutoka shule jirani wakisoma barua kutoka kwa wapenzi wao katika shule ya Starehe Naye Stephanie aliniarifu kuwa alifurahishwa sana na barua aliyopokea, '' alinifurahisha sana naona alitumia lugha safi sana, naona tuendelee matumizi ya barua'', anasema. Nilimtaka msichana Angel kunieleza kilichomvutia zaidi katika barua aliyopokea. '' Nilifurahia pale aliponiambia kuwa nywele zangu ndefu zinapendeza na kwamba nina tabasamu ya kuvutia kiasi kwamba inaweza kumfanya awe kipofu'' anasema huku akicheka. Huku vijana wengine duniani wakiwasiliana na marafiki zao kwa kutumia simu za mkononi imebidi sisi kutumia mbinu ya kuandika barua kufanya hivyo na inatufaa na kutufurahisha.

BBC.

KENYA AIRWAYS YAPUNGUZA SAFARI ZA TZ.

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways leo limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika hilo kupunguza safari zake kutoka 42 kwa wiki hadi 14. Serikali ya Tanzania inasema huo ndio mkataba wa tangu awali na kulaumu mamlaka ya anga nchini Kenya kwa kushindwa kuafikia maelewano na mamlaka ya Tanzania kuhusu jambo hilo. Tayari baadhi ya wasafiri wanaotumia ndege za shirika hilo wameanza kuathirika kufuatia shirika hilo kufuta baadhi ya safari kutoka Dar es Salaam.

BBC.